Posts

Super Morsa

Image
           Uwiiiiii aiiiiiiii jaman nakufaaaaa........Alora alilala chini akiugulia maumivu makali kutokana na kipigo cha mumewe Chiumbo. Mlango ulikuwa umefungwa, hakuna jirani aliyeweza kumwokoa Alora. Aidha tegemeo la pekee lingekuwa mtoto aliyeko tumboni, ambaye Alora humwimbia nyimbo na kumsihi awahi kuzaliwa ili Alora apate rafiki.Alora aliugulia maumivu makali kila kona ya mwili wake. Aliikinga mikono yake tumboni ili mateke ya Chiumbo yasimdhuru mtoto.Chiumbo alipochoka kumpiga Alora mateke, alianza kumpiga na kila alichokiona mbele yake.Alimpiga kila sehemu. Alora sio mda alianza kuona giza, aliona kila kitu kilichomzunguka kinabadilika na kuwa cheusi. Alianza kulegea hadi kulala chini kabisa.  Alizimia. Chiumbo aliyekuwa anayumba huku na kule kwa pombe kali kichwani alifungua mlango na kutoka nje. Alichukua ndoo ya maji na kwenda kumwagia Alora mwili mzima.  Alora alifungua macho haraka kama mtu aliyetoka kwenye usingizi wenye ndoto mbay...

K A S R I

Image
 Mfalme Duncan alikuwa akipigana vita kwa takribani miezi sita kwa ajili ya kulinda jiji la Haven. Jiji hili lilikuwa na watu wengi, uongozi wake ulikuwa imara na jeshi lisilopigwa na maadui zake. Wakazi wengi ambao ni wazaliwa na wahamiaji kutoka vijiji jirani, hujishughulisha na shughuli mbalimbali. Ni kijiji tajiri kwa madini na kilimo. Hata hivyo, kutokana na utajiri wa wananchi wake, watoto huzaliwa wakiishi katika mazingira mazuri. Wazee huozesha binti zao kwa kupokea mahari za dhahabu na Vito vingi vya thamani. Hata hivyo, sio rahisi kuingia katika himaya hii ya kifalme yenye sheria kali.  Baada ya kutoka vitani Mfalme aliwaita wake zake watatu; Charlotte , Helena na Victoria pamoja na watoto wake wote ; Elsa, James, Albert, Rose na Belle. Charlotte, aliyevaa gauni refu, la njano, ni mke wa kwanza wa Mfalme Duncan, ana watumishi wapatao mia moja kwa ajili ya kumuhudumia kwa kila atakachohitaji. Charlotte ni mpiganaji vita, aliolewa baada ya baba yake kushindwa vita na ...
Image
 Taja kitabu changu unachopenda cover lake. Taja unachotamani kukisoma Bure  Offer ya masaa matano Tu.

Chakula gani usichopenda? Kwanini?

Image
 

Vocha sh 5000 ya bure kwa mshindi.

Image
 Makala ipi umeipenda katika blog hii? Mwenye sababu nzuri zaidi atatuma namba kisha atapata vocha ya bure kwa mtandao anaotumia. Toa comment hapo.

UZEE KWISHA!!!

Image
  Je ulishawahi kutumia Rosela? Kwenye mazingira gani? Kwanini? Katika faida mamia za rosela, basi jifunze hii mojawapo. Rosela ni Anti-aging. Inazuia mikunjo kwenye ngozi. Matumizi ya kila siku ya roselle iliyotengenezwa inaweza kuboresha unyevu wa ngozi na kupunguza mikunjo, kulingana na utafiti kutoka Taiwan. Utafiti mmoja uliofanya chuo kikuu cha Chung Shang, iligundua kuwa matumizi ya kila siku ya 200ml ya kinywaji cha roselle kilichotengenezwa iliweza kuongeza uwezo wa kuhifadhi maji ya ngozi na kupunguza mikunjo. Utafiti huo uliochukua miezi mitano, ulihusisha takriban watu 60 wenye umri wa miaka 25 hadi 85 kutoka hospitali na mazingira ya jamii. Hii inaweza kuwa kutokana na jukumu la aina mbalimbali za "phytochemicals" zinazopatikana katika maua ya roselle. Utahitaji kuchemsha maua ya Roselle na kunywa maji yake. Baada ya kuchemsha, kemikali zote muhimu zilizopo kwenye Roselle kama vile phytochemicals zitatolewa na kufanya kazi mwilini.     

FAHAMU KUHUSU TANGAWIZI

Image
Faida za Tangawizi kiafya 1. Inapambana na Vijidudu Baadhi ya kemikali katika tangawizi mbichi husaidia mwili wako kuzuia vijidudu. .ni wazuri sana katika kuzuia ukuaji wa bakteria.  2. Hufanya Kinywa chako kiwe na Afya Nguvu ya antibacteria ya tangawizi inaweza pia kuangaza tabasamu lako. Virutubisho vinavyofanya kazi katika tangawizi vinayoitwa gingerols huzuia bakteria  mdomoni kukua. .bakteria hawa ni wale wale ambao wanaweza kusababisha ugonjwa wa periodontal, maambukizi makubwa ya fizi. 3.Inatuliza Kichefuchefu Hadithi ya wake wa zamani inaweza kuwa ya kweli: Tangawizi husaidia ikiwa unajaribu kupunguza tumbo lililovurugika haswa wakati wa ujauzito. .inaweza kufanya kazi na kukusaidia kuondokana na gesi iliyojaa kwenye matumbo. Inaweza pia kusaidia kutatua tatizo la kichefuchefu 4.Hutuliza maumivu makali ya Misuli. Tangawizi haitaondoa maumivu ya misuli papo hapo, lakini inaweza kudhibiti maumivu baada ya muda. Katika tafiti zingine, watu wenye maumivu ya misuli kutokana...